• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • SOKA: Real Madrid yajizatiti kumsajili Sterling wakitumia mwanya wa City kufungiwa kwa miaka miwili

    (GMT+08:00) 2020-02-17 10:43:11

    Miamba ya soka ya La Liga nchini Hispania, Real Madrid inatarajia kuongeza juhudi zake za kumsajili mchezaji, Raheem Sterling wakitumia mwanya wa Manchester City kufungiwa kwa muda wa miaka miwili na UEFA kutoshiriki michuano ya Champions League. Habari mbaya zaidi kwa mabingwa hao wa Premier League ni kuwa Juventus sasa itaongeza juhudi zake za kumng'oa kocha wa klabu hiyo Pep Guardiola. Miamba hiyo ya Hispania, Real tayari ipo kwenye mipango ya kutoa dau la paundi milioni 180, hii ikiwa ni kabla hata ya taarifa hizo za kushitua za kufungiwa kwa City. Sterling mwenye umri wa miaka 25, ana mkataba wa miaka mitatu wa kuwa katika dimba la Etihad huku mazungumzo yakiendelea tangu mwezi Novemba kuhakikisha anaongezewa mapato yake ya wiki kutoka paundi 300,000 hadi kufikia 450,000.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako