• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • SOKA: Aston Villa yasalimu amri mbele ya Tottenham, yacharazwa mabao 3-2

    (GMT+08:00) 2020-02-17 10:43:34

    Aston Villa imekubali kichapo cha mabao 3-2 mbele ya Tottenham, kwenye mchezo wa Ligi Kuu England uliochezwa jana usiku kwa kufungwa bao katika dakika za nyongeza. Toby Alderweireld alichanganywa na Mbwana Samatta na kujifunga bao dakika ya 9 lililosawazishwa na yeye mwenyewe Toby dakika ya 27. Kabla ya mapumziko Villa ilijichanganya na kufungwa bao la pili na Son Heung-min dakika ya 45+2 akimalizia penalti iliyopanguliwa na mlinda mlango wa Villa. Mapumziko Spurs ilikuwa inaongoza kwa mabao 2-1 kipindi cha pili Bjorn Engels aliweka mzani sawa dakika ya 53 lilidumu mpaka dakika ya 90. Hii inakuwa mechi ya pili kwa Mbwana Samatta kucheza ndani ya Ligi Kuu England baada ya kujiunga na Villa akitokea klabu ya Genk. Balaa lilipatikana dakika ya 90+4 kwa Son kutupia bao la tatu na la ushindi Kwa Spurs liliwamaliza nguvu Villa. Aston Villa ipo nafasi ya 17 ikiwa na pointi zake 25 na Spurs nafasi ya tano ikiwa na pointi 40 zote zimecheza mechi 26.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako