• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • SOKA: Twiga Stars yaendelea kufanya vizuri Kombe la UNAF kwa kuinyuka Algeria mabao 3-2

    (GMT+08:00) 2020-02-17 10:43:57

    Timu ya Soka ya Taifa ya Wanawake ( Twiga Stars) imeendelea kufanya vizuri katika mashindano ya Kombe la UNAF baada ya kupata ushindi wa mabao 3-2 dhidi ya Algeria katika mchezo uliochezwa jana kwenyee Uwanja wa Kram jijini Tunis nchini Tunisia. Kwa ushindi huo, Twiga Stars imefikisha pointi sita na kuongoza katika msimamo wa mashindano hayo yanayoshirikisha nchi tano za Kanda ya Kaskazini na Tanzania wakiwa wageni waalikwa. Twiga Stars itashuka tena dimbani leo kucheza dhidi ya Morocco ambayo nayo iliwafunga Tunisia katika mchezo wa kwanza na itamaliza dhidi ya wenyeji hao Februari 22, mwaka huu. Juzi jioni Tunisia ilishuka dimbani kuwakaribisha Mauritania, timu zote zikiwa na kumbukumbu ya kufungwa katika mechi zao za kwanza.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako