Benki ya Dunia imeishauri serikali ya Uganda kufanya uwekezaji zaidi katika maendeleo ya mitaji ya watu, ikisema ni muhimu kuwekeza kwa watoto na vijana ili kuinua viwango vya maisha.
Uganda inapaswa kupanua ulinzi wa kijamii kwa kusaidia uwekezaji katika uwekezaji wa binadamu na, kuwa makini katika mipango ya kulinda jamii katika kuboresha uvumilivu na fursa za kiuchumi.
Kukosekana kwa usawa wa mapato kunaathiri uchumi na jamii, na ushahidi unaokua unaonyesha kwamba ukosefu mkubwa wa usawa unaweza kuwa mbaya kwa ukuaji.
Kuna pia wasiwasi kwamba ukosefu wa usawa unaweza kupunguza fursa za masomo na utulivu wa jamii.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |