• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Serikali ya Tanzania imepokea mkopo wa Sh bilioni 147 kutoka Benki ya Standard Chartered

    (GMT+08:00) 2020-02-17 19:23:46

    Serikali ya Tanzania imepokea mkopo wa Sh bilioni 147 kutoka Benki ya Standard Chartered Tanzania kufadhili ujenzi wa mradi wa Standard Gauge Railway (SGR).

    Waziri wa Fedha na Mipango wa Tanzania Philip Mpango amesema fedha hizo zitatumika kujenga reli ya kati yenye urefu wa kilomita 550 inayounganisha Dodoma na Dar es Salaam kupitia Morogoro na Makutupora.

    Mara tu reli hiyo itakapo kamilika, watanzania watapata njia bora ya usafiri na usafirishaji wa mizigo kutoka na kuenda kwa Bandari ya Dar es salaam

    Serikali ya Tanzania inatarajia reli hiyo kushughulikia changamoto za sasa za msongamano na kupunguza malipo ya huduma ya usafirishaji kwa asilimia 40.

    Tanzania inatarajia SGR iunganishe nchi na mataifa jirani ya Burundi, Rwanda na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, DRC, hivyo inachukua jukumu muhimu katika kukuza biashara ya kikanda.

    Kulingana na serikali ya Tanzania, mradi huu tayari umeunda zaidi ya fursa 8,000 za ajira za moja kwa moja kwa watanzania na imefungua fursa kwa jamii zilizo karibu na eneo la mradi huo kupata huduma za kijamii kama makazi na chakula.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako