• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • TUZO: Tuzo za Laureus zaenda kwa Simone Biles, Lewis Hamilton na Lionel Messi

    (GMT+08:00) 2020-02-18 08:26:10

     

    Simone Biles ameshinda tuzo yake ya tatu ya Laureus ya mwanamichezo bora wa kike wa mwaka (Laureus Sportswoman) huku bingwa wa Formula 1 Lewis Hamilton na msakata kabumbu Lionel Messi wakishinda taji la wanaume. Mmarekani Biles, mwenye miaka 22, mwaka jana alishinda medali tano za dhahabu huko Stuttgart na kuwa mwanariadha aliyeng'ara zaidi kwa mabingwa wa dunia. Muingereza Hamilton, mwenye miaka 35, ameshinda taji lake la sita la udereva. Na Muargentina Messi, mwenye miaka 32, ameiongoza Barcelona kubeba kombe la La Liga kwa mara yake ya kumi. Akiongea baada ya kushinda tuzo hiyo Hamilton amesisitiza kuwa katika F1 hakuna mchangamano. Na amesema ni changamoto wanayoikabili kila siku, hata hivyo amesema ni jukumu lao kutumia jukwaa hilo kuhamasisha usawa wa kijinsia na kushirikisha zaidi wanawake kwenye mbio za Formula 1.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako