• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Ziwa Victoria imejaa sumu na kinyesi.

    (GMT+08:00) 2020-02-18 18:17:23

    Utafiti wa hivi punde kuhusu uchafuzi wa maji ya Ziwa Vitoria huenda ukaathiri pakubwa mno biashara ya samaki waoavuliwa kutoka ziwa hilo. Hii ina maana kwamba, mataifa ya Afrika Mashariki yataathirika pakubwa huku maelfu ya watu wanaotegemea biashara hiyo watapoteza wateja wao.

    Ripoti za uchunguzi wa mahabara zinaonyesha kwamba samaki wanaovuliwa kutoka Ziwa Victoria wana madini ambayo ni sumu kwa mwili wa mwanadamu.

    Sampuli za maji zilizopimwa zilionyesha kuwa asilimia 92 ya Ziwa Victoria imechafuka hasa kutokana na kinyesi cha binadamu na madini yenye sumu.

    Iligunduliwa pia kuwa mito ipatayo 10 inayomimina maji ziwani humo pia inamwaga virusi vinavyoweza kusababisha magonjwa.

    Samaki wote waliochunguzwa walipatikana kuwa na aina mbalimbali za madini ambayo ni pamoja na risasi, cadmium, chromium, zinc, iron, copper na manganese.

    Hata hivyo, baadhi ya madini hayo ni ya viwango vinavyokubalika kiafya. Lakini samaki waliovuliwa katika ufuo wa Marenga nchini Kenya, Masese na Gabba nchini Uganda walipatikana kuwa na viwango hatari vya risasi.

    Madini ya risasi husababisha saratani, uhaba wa damu na nguvu mwilini pamoja na madhara ya figo na ubongo.

    Kwenye ziwa, maji katika eneo la Homabay yalipatikana kuwa chafu zaidi ikifuatwa na yale ya Kendu Bay, Mto Sondu na ufuo wa Kisumu. Hii inatokana zaidi na umwagaji wa taka.

    Kulingana na uchunguzi huo wa kina ulioshirikisha wanasayansi, Ziwa Victoria, ambalo ndilo kubwa zaidi Afrika lina uchafu na sumu ambazo zimesababisha kuangamia kwa aina kadhaa za samaki.

    Uchafuzi huo ni mwingi zaidi karibu na nchi kavu kuliko kati mwa ziwa.

    Kati ya dawa za kuua wadudu zilizopatikana ni DDT ambayo imepigwa marufuku nchi zingine kwa kusababisha kansa, endosulfan inayodhuru watoto wachanga na mirex ambayo pia husababisha saratani.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako