• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Afrika mashariki kuweka mikakati ya kuthibiti biashara haramu ya dhahabu.

    (GMT+08:00) 2020-02-18 18:17:46

    Mataifa ya ukanda wa Afrika Mashariki yanajadiliana jinsi ya kukomesha biashara haramu ya dhahabu. Shughuli za kimagendo za dhahabu zimekita mizizi sana kwa mataifa ya Afrika Mashariki na Kati, huku bidhaa hiyo ikipitishwa na kuuzwa ughaibuni.

    Maafisa wanaowakislisha wachimbaji dhahabu kutoka mataifa ya Afrika Mashariki, wamepanga kukutana mwezi ujao ili kuweka mikakati kuhusu biashara ya dhahabu. Kando na hilo, watajadiliana jinsi ya kupeana leseni kwa wachimbaji dhahabu na namna ya kutoza ushuru kwa bidhaa hii. Yote haya, yamepangiwa kuanza kutekelezwa katikati ya mwaka huu.

    Taifa la Congo ni mojawapo ya mataifa ambayo dhahabu huuzwa nje kimagendo kupitia mataifa majirani.

    Endapo mataifa ya Afrika Mashariki na Kati yatakubaliana kuhusu marekebisho haya, basi sekta ya dhahabu itaimarika na kusaidia ukuaji wa uchumi wa ukanda huu.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako