• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Uganda: Viwanda na makampuni kubwa hayauzi bidhaa zao Rwanda.

    (GMT+08:00) 2020-02-18 18:18:25

    Watengenezaji bidhaa wa viwanda vikubwa nchini Uganda, hawasafirishi bidhaa zao nchini Rwanda kama ilivyokuwa hapo awali. Bidhaa kama vile saruji, vyuma na mabati havipati mwanaya wa kuingia Rwanda huku serikali za mataifa haya mawili zikijitahidi kurahisisha mambo.

    Kampuni za kutengeneza bidhaa za kuezeka nyumba, ile ya Saruji ya Hima na Movit, ni baadhi ya watengenezaji ambao wameathirika pakubwa baada ya mpaka wa Rwanda na Uganda kufungwa mwezi Februari mwaka uliopita.

    Kulingana na gazeti kuu nchini Uganda, watengenezaji wa bidhaa hizi wanasema kwamba licha ya kuwa hakuna yeyote anayewazuia kuingia nchini Rwanda, kuingiza bidhaa zao nchini humo ndio kazi ngumu. Aidha njia zingine zilizopo, ni ghali mno kwao.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako