• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • SOKA: Mshambuliaji wa Tottenham Son Heung-min nje kwa wiki kadhaa baada ya kuvunja mkono

    (GMT+08:00) 2020-02-19 10:48:54

    Mshambuliaji wa Tottenham Son Heung-min atakuwa nje ya uwanja kwa wiki kadhaa baada ya kuvunja mkono katika mechi ya Jumapili waliyoshinda 3-2 dhidi ya Aston Villa. Mchezaji huyo raia wa Korea Kusini ambaye ana miaka 27, atafanyiwa upasuaji wiki hii. Hii ina maanisha atakosa mchezo wa Ligi ya Mabingwa hatua ya 16 bora dhidi ya RB Leipzig leo Jumatano na mechi dhidi ya ligi ya Premier dhidi ya Chelsea itakayochezwa Jumamosi. Tottenham tayari wamemkosa straika wa England Harry Kane, aliyejeruhiwa mguuni mwezi Januari walipocheza na Southampton.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako