• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China yarahisisha taratibu za kibiashara kwa nchi za kigeni

    (GMT+08:00) 2020-02-19 18:22:54

    China imesema iko kwenye harakati ya kurahisisha taratibu za kibiashara kwa wawekezaji wa kigeni walio nchini humo, ili warejee shughuli zao za biashara kama kawaida, wakati huu wa mlipuko wa virusi vya korona.

    Kwa mujibu wa taarifa iliyochapishwa mitandaoni na Wizara ya Biashara ya China Jumanne wiki hii, serikali ya China itasaidia makampuni yanayoshughulikia biashara na nchi za nje, uwekezaji wa kigeni na biashara ya mitandaoni chini ya pendekezo la Njia Moja na Ukanda Mmoja.

    Wizara ya Biashara ya China itazisaidia biashara hizo za kigeni haswa katika kuongeza uzalishaji wa bidhaa, kuwaunga mkono wafanyabiashara wa kigeni kuagiza dawa na vyakula vya shambani kutoka nchi nyingine, ambazo ni bidhaa zinazohitajika sana hivi sasa nchini China.

    Kulingana na taarifa hiyo ya Wizara ya Biashara ya China, kampuni za kibiashara zitakazopewa kipaumbele ni zile zinazohusiana na uuzaji na usambazaji wa bidhaa muhimu za kinga kama vile vichuja hewa, kemikali za kuua viini vya maradhi, glavu za kujikinga, miwani ya kukinga macho nk.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako