• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Tanzania yapendezwa na kasi ya viwanda

    (GMT+08:00) 2020-02-19 18:42:30
    Serikali ya Tanzania imesema inapendekezwa na kasi ya viwanda na kuahidi kuweka mazingira rafiki ya uwekezaji. Akizungumza wakati akitembelea baadhi ya viwanda katika Halmashauri ya Mji wa Kibaha, waziri wa viwanda na Biashara, Innocent Bashungwa, pia alieleza namna alivyoridhishwa na halmashauri hiyo inavyotekeleza sera ya uwekezaji wa viwanda kwa vitendo. Akiwa katika kiwanda cha kuunganisha mabasi makubwa kinachomilikiwa na Kampuni ya BM Motors, alimpongeza mwekezaji wa Kitanzania kwa uwekezaji wake wenye tija.

    Alisema, kitendo cha mwekezaji huyo mzawa kuwekeza nchini humo, ni manufaa kwa Taifa katika suala la kodi, ajira kwa Watanzania, lakini ni fursa kwa viwanda vingine kwani malighafi zinazotumika zinapatikana nchini humo.

    Mbali ya kiwanda hicho, Waziri Bashungwa pia alitembelea kampuni ya wawekezaji wazawa ya GF Vehicle Assemblies kilichopo eneo la Tamco.

    Kampuni hiyo inatarajia kuanza kuunganisha magari mchanganyiko yenye uzito usiozidi tani nane ambapo uzinduzi wake unatarajiwa kufanyika Mei mwaka huu.

    Bashungwa aliwapongeza wawekezaji waliowekeza nchini, huku akitoa rai kwa mamlaka na taasisi zinazohusika na viwanda vidogo vidogo zikiwamo SIDO, DIT na NEMC kuwa karibu na wawekezaji kwa ushauri wa kitaalamu.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako