• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • DRC yatoa mpango wa matumizi ya fedha

    (GMT+08:00) 2020-02-19 18:42:50

    Serikali ya DRC imetoa mpango wa matumizi ya fedha utaosaidia kurekebisha matumizi ya serikali, baada ya kupotea kwa Mamilioni ya dola mwaka 2019.

    Hivi majuzi shirika la Fedha Dunia (IMF) liliitaka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) kuonyesha ukweli katika matumizi yake ya fedha za uma.

    Mbali na bajeti ya kihistoria ya kiwango cha juu ya dola bilioni 11, zilizotangazwa miezi miwili iliyopita na rais Tshisekedi, mpango huo wa kuzuia pesa kupotea umeokoa nusu ya mapato pamoja na matumizi ya fedha.

    DRC imepanga kutumia dola bilioni 5.64 na serikali inaamini inaweza kupata dola bilioni 5.4 katika mapato yake. Upungufu wa milioni 200 unatarajiwa kujazwa na fedha zitakazotolewa na Benki Kuu.

    Uchunguzi kuhusu matumizi ya pesa yanayo fanyika ikulu nchini DRC, ulibaini kwamba ikulu ilitumia pesa nyingi kwa kipindi cha muda mchache kiasi kwamba, tangu rais Felix Tshisekedi aingie madarakani, pesa zinazotakiwa kutumika ikulu kwa muda wa mwaka mzima, zilitumika na kuisha kabisa kwa muda wa miezi 5 pekee ambayo rais amekaa madarakani.

    Kesi ya kupotea kwa Dola Milioni 15 ilizua hali ya sintofahamu nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, huku mashirika ya kiraia yakiomba uchunguzi wa kina ufanyike ili kupata ukweli wa mambo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako