• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Tullow yasema haijafiliska

    (GMT+08:00) 2020-02-19 18:46:29

    Kampuni ya uchimbaji mafuta nchini Kenya Tullow imekanusha taarifa kuwa imefilisika. Taarifa hiyo inakuja siku moja tu baada ya gazeti moja nchini Kenya kutangaza kuwa kampuni hiyo imefilisika na hivi sasa haiwezi kutekeleza shughul;I zake za mafuta. Hata hivyo Tullow imesema lengo lake kuu hivi sasa ni kuhakikisha inaiweka Kenya katika daraja la nchi zinazouza mafuta katika soko la kimataifa.Katibu mkuu mtendaji wa Tullow Martin Mbogo amesema Kenya bado mafuta ya Kenya bado yana thamani kubwa ya kiuchumi na nia yao ni kuendelea kuwekeza zaidi katika sekta hiyo nchini Kenya.Taarifa ya gazeti hilo ilisema kuwa Tullow hivi sasa inalemewa na madeni mengi jambo ambalo huenda likapelekea waanze mikakati ya kupunguza gharama ikiwemo kuwaachgisha kazi baadhi ya wafanya kazi wake.Tullow inadai kuwa walilazimika kukatiza baadhi ya shughuli zake kwa muda kufuatia mvua kubwa ambayo ilikuwa imenyesha na kuharibu barabara. Hivi sasa usafirishaji wa mafuta kwa kutumia malori umesitishwa hadi pale barabara zitakaporekebishwa.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako