• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Tanzania yawataka vijana kuchangamkia mikopo, zawadi fedha, bodaboda

    (GMT+08:00) 2020-02-19 18:46:58

    Serikali ya Tanzania imewataka vijana nchini humo kuchangamkia fursa za mikopo na zawadi za fedha taslimu na bodaboda kwa lengo la kurasimisha biashara zao.

    Waziri wa nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Jenista Mhagama, amesema sekta ya bodaboda kwa sasa inaheshimika na kutambulika kama ajira rasmi, hivyo wahusika hawana budi kutumia fursa hiyo kujinufaisha.

    Kupitia kampeni ya mastaboda, waendesha bodaboda wamerasimishwa, hivyo kuaminika na kupewa msaada kupitia mikopo ya fedha hata ya vyombo vya kazi kama pikipiki za miguu miwili na miguu mitatu.

    Mhagama alisema kwa sasa serikali inatambua sekta hiyo kuwa rasmi na kuahidi vijana wote nchini humo kuwa serikali itaendelea kuweka mazingira wezeshi kwa kushirikiana na wabia kama Benki ya NMB.

    Alisema asilimia 56 ya nguvukazi nchini humo ni vijana na ajira rasmi hivi sasa ni chache, hivyo kuwataka vijana kutafuta mifumo tofauti ya ajira na kujiajiri au kusaidiwa kutengeneza ajira.

    Kiongozi wa bodabada ambaye amehitimu chuo kikuu na kukosa ajira rasmi, alisema hadi kufikia mwaka 2019, idadi ya madereva bodaboda katika Mkoa wa Ruvuma ilifikia 85,000.

    Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma, Pololet Mgema, aliipongeza benki hiyo kwa kuanzisha huduma hiyo ambapo amewaomba waendesha bodaboda kujiunga sambamba na kuchukua vitambulisho vya wajasiriamali ili kupata mkopo kutoka benki hiyo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako