• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China ina uwezo wa kutimiza lengo la kuondoa umaskini

    (GMT+08:00) 2020-02-20 17:23:30

    Mjumbe wa taifa wa China ambaye pia ni waziri wa mambo ya nje Bw. Wang Yi amekutana na rais Bounnhang Vorachit wa Laos na kusema, ana imani kuwa China ina uwezo wa kutimiza lengo lake la kuondoa umaskini kabla ya mwaka kesho.

    Akishiriki kwenye mkutano maalum wa mawaziri wa mambo ya nje wa nchi za ASEAN kuhusu kushirikiana kupambana na virusi vya korona COVID-19, Bw. Wang amesema, China inashukuru misaada iliyotolewa na serikali na watu wa Laos ambayo imeonesha urafiki mzuri kati yao.

    Bw. Wang pia amesema, China ina imani ya kushinda mapambano hayo kutokana na ubora wa mfumo wa ujamaa wenye umaalumu wa China na uzoefu mkubwa katika kushughulikia masuala ya afya ya umma. Pia anatarajia nchi hizo mbili zitaendelea kusukuma mbele mchakato wa kiviwanda na kuongeza ushirikiano wa kunufaishana wa sekta mbalimbali, ili kuwanufaisha zaidi watu wa nchi hizo mbili.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako