• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Korea Kusini yapeleka balozi mpya mjini Wuhan

    (GMT+08:00) 2020-02-20 17:23:59

    Msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya China Bw. Geng Shuang amesema, hatua ya Korea Kusini kupeleka balozi mpya mjini Wuhan, imeonesha nchi hiyo inaiunga mkono China katika kipindi hiki muhimu cha kupambana na virusi vya korona COVID-19.

    Bw. Geng amesema, kitendo hicho kimeonesha Korea Kusini inazingatia uhusiano na China, na China inapenda kumsaidia balozi huyu kuanza kazi zake kwa urahisi.

    Bw. Geng pia amesema, tangu kutokea kwa mlipuko wa virusi hivyo, serikali na jamii ya Korea Kusini imetoa misaada mingi kwa China. Watu wa Korea Kusini pia wametoa misaada ya fedha kupitia ubalozi wa China nchini humo kuwasaidia wachina kushinda mapema mapambano hayo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako