• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Msemaji wa Wizara ya mambo ya nje ya China akanusha kauli ya waziri wa mambo ya nje wa Marekani

    (GMT+08:00) 2020-02-20 18:21:20

    Waziri wa mambo ya nje wa Marekani Bw. Mike Pompeo ameishutumu China kwa kuwafutia waandishi watatu wa habari kadi zao, na kusema kuwa kitendo hicho kimeweka vizuizi kwa uhuru wa kutoa maoni.

    Akijibu kauli hiyo kupitia mtandao wa Internet, Msemaji wa Wizara ya mambo ya nje ya China Bw. Geng Shuang amesema, suala hilo halihusiani na uhuru wa kutoa maoni kama alivyodai Bw. Pompeo. Amesema Gazeti la The Street Journal lilitoa makala inayoipaka matope China na kuchochea ubaguzi, na kwamba makala hiyo inakwenda kinyume na ukweli wa maadili na taaluma, ambayo imezusha hasira kubwa ya wachina na kulaumiwa na jumuiya ya kimataifa.

    Pia amesisitiza kuwa, China inashughulikia masuala ya waandishi wa habari wa kigeni kwa kufuata sheria na kanuni zinazohusika, na vyombo vya habari vinavyotoa kauli za kudhalilisha China, kuchochea ubaguzi au kupata matope China hakika vitaadhibiwa.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako