• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Benki ya Dunia yasema, msaada wa fedha wa kigeni unaingia mifukoni mwa watu mashuhuri wa nchi maskini

    (GMT+08:00) 2020-02-20 18:23:16

    Benki ya Dunia imesema kuna ushahidi kuwa msaada wa fedha wa kimataifa umeingia kwenye mifuko ya watu mashuhuri katika nchi zilizopokea msaada huo.

    Katika makala yake iliyotoa Jumanne wiki hii iitwayo "Watu Mashuhuri Wakamata Msaada wa Kigeni: Ushahidi kutoka Akaunti za Benki za Nje ya Nchi", Benki ya Dunia imepitia mikopo iliyotoa kwa nchi 22 zinazoendelea ambazo zinategemea zaidi msaada kutoka nje katika kipindi cha kuanzia mwaka 1990 hadi mwaka 2010, na kwamba karibu asilimia 7.5 ya mikopo hiyo ilidhibitiwa na watu mashuhuri wa nchi hizo na kuingia kwenye akaunti zao za benki za nje ya nchi husika.

    Makala hiyo inasema, robo moja ya nchi zilizopokea msaada kutoka nje imepokea msaada uliochukua asilimia moja ya pato la taifa GDP, lakini kasi ya ongezeko la fedha zilizo katika akaunti za benki za nje za nchi hizo ilifikia asilimia 3.4 ikilinganishwa na nchi ambazo hazikupata msaada kutoka nje. Utafiti umeonesha kuwa, msaada wa fedha uliotolewa kwa nchi hizo zinazotegemea zaidi msaada kutoka nje zinalingana na fedha zilizoongezeka katika akaunti za benki za nje ya nchi hizo, na wakati wa fedha zilipoingia kwenye akaunti za benki za nje ya nchi hizo ndio wakati msaada wa fedha ulipofika katika nchi hizo.

    Hitimisho lililopatikana ni kuwa, msaada wa fedha wa kimataifa umedhibitiwa na wanasiasa, maofisa na watu wenye uhusiano nao.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako