• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kauli kuhusu virusi vya COVID-19 vinatokana na mpango wa "vita vya kikemikali" wa China haina msingi wowote

    (GMT+08:00) 2020-02-20 19:20:28

    Msemaji wa Wizara ya mambo ya nje ya China Bw. Geng Shuang amesema, China inatumai kuwa wakati jumuiya ya kimataifa inapopambana kwa pamoja kukabiliana na ugonjwa mpya wa COVID-19, itaendelea kupambana na kuzuia kwa pamoja "virusi vya njama mbalimbali za kisiasa".

    Hivi karibuni, baadhi ya watu na vyombo vya habari vya nchi za magharibi vilidai kuwa virusi vipya vya COVID-19 ni "silaha za kikemikali" ambavyo vilitoka kwenye maabara moja nchini China. Bw. Geng amesema, hivi sasa watu wa China wanapambana na virusi hivyo kwa nguvu zote, hali ambayo inajiwajibika na pia inawajibika na usalama wa afya ya umma duniani. Amesema kitendo cha baadhi ya watu na vyombo vya habari kutoa kauli kama hizo zinazochochea hofu kina nia mbaya ama kukosa elimu ya kimsingi.

    Bw. Geng amesema, hivi karibuni maofisa wa Shirika la Afya Duniani WHO wametangaza mara kwa mara kuwa, hakuna ushahidi wowote kuwa virusi hivyo vilitengenezwa katika maabara au kusababishwa kutokana na utengenezaji wa silaha za kikemikali.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako