• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Serikali ya Tanzania kuja na sera ya kilimo kuinua sekta hiyo

    (GMT+08:00) 2020-02-20 19:58:57

    Naibu Waziri wa Kilimo Tanzania, Hussein Bashe, amesema serikali inatarajia kuja na sera ya kilimo ambayo inalenga kuinua sekta hiyo.

    Akizungumza katika Kongamano la sita la wadau wa sera za kilimo, mifugo na uvuvi, Bashe alisema sera hiyo itakuwa mkombozi mkubwa kwa mkulima.

    Alisema kilimo ni sekta iliyoajiri wananchi wengi na ukuaji wa sekta ya kilimo ni asilimia 5.3.

    Hata hivyo, alisema wanataka vyama vya ushirika vifanye kazi na kutoa matokeo yaliyokusudiwa.

    Aidha, Bashe alisema serikali iko tayari kuendeleza sekta binafsi kwa kuwa ndiyo inayochangia pato la Taifa kwa asilimia kubwa katika sekta mbalimbali ikiwamo ya kilimo.

    Kwa upande wake, Makamu Mwenyekiti wa Baraza la Kilimo Tanzania, Jitu Soni, alisema Tanzania imekuwa ikitumia mbolea kwa kiwango kidogo sana ikilinganishwa na nchi ya Kenya.

    Alieleza kuwa kiasi ya kilo 18 kwa hekta kimekuwa kikitumika kwa Tanzania huku Kenya ni wastani wa kilo 50 kwa hekta.

    Akizungumzia utafiti uliofanyika kwenye mikoa tisa nchini Tanzania kwa misimu mitatu ya kilimo, Soni alisema ilibainika kuwa usambazaji wa mbolea kutoka Dar es Salaam kwenda kwa wakulima mikoani, bei elekezi ilishindwa kufuatwa kutokana na kero za usafiri.

    Mwenyekiti wa timu ya wachambuzi wa sera na Mkurugenzi Mtendaji wa Jukwaa la wadau wa kilimo wasio wa kiserikali (ANSAF), Audax Rukonge, alisema bado kiwango cha mbolea kinachotumika kwenye mashamba ni kidogo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako