• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Serikali ya Kenya yapanga kupunguza matumizi katika mwaka wa fedha 2020/2021

    (GMT+08:00) 2020-02-20 19:59:24

    Serikali ya Kenya inapanga kupunguza matumizi yake katika mwaka wa kifedha ujao unaoanza mwezi Julai 2020 kwa kiwango cha asilimia 23.6 ya jumla ya pato la taifa (GDP) kutoka asilimia 26 mwaka huu wa kifedha.

    Haya yametangazwa na Wizara ya Fedha katika hati ya kisera ya bajeti.

    Wizara ya Fedha inasema hatua ya kupunguza matumizi inalenga kuisaidia serikali kupunguza pengo katika bajeti kwa kupindi hicho hadi asilimia 4.9 ya GDP.

    Katika mwaka huu wa kifedha pengo katika bajeti ni asilimia 6.3 ya GDP.

    Serikali inapanga kukopesha Sh222.9 bilioni kutoka mashirika ya kifedha ya humu nchini kuziba pengo katika bajeti.

    Aidha taarifa hiyo inayojadiliwa na kamati mbalimbali za Bunge inasema kuwa serikali inapanga kukopa Sh345.1 bilioni kutoka mashirika ya kifedha kutoka nje.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako