• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Rais Xi Jinping wa China afanya mazungumzo kwa njia ya simu na viongozi wa Korea Kusini na Pakistan

    (GMT+08:00) 2020-02-20 20:41:10

    Rais Xi Jinping wa China leo amefanya mazungumzo kwa njia ya simu na rais Moon Jae-in wa Korea Kusini.

    Katika mazungumzo yao, rais Xi amesema China inaishukuru serikali na jamii ya Korea Kusini kwa kutoa misaada kwa China tangu kutokea kwa mlipuko wa virusi vipya vya korona COVID-19 nchini China. Amesema China itaendelea kufuata msimamo wazi, kuimarisha mawasiliano na ushirikiano na nchi mbalimbali ikiwemo Korea Kusini, kupambana kwa pamoja ugonjwa huo ili kunufaisha afya ya watu duniani.

    Kwa upande wake, rais Moon Jae-in amesema Korea Kusini itaendelea kutoa misaada kwa China katika mapambano dhidi ya ugonjwa huo, na kuimarisha ushirikiano kati ya pande hizo mbili katika sekta ya afya.

    Katika mazungumzo na waziri mkuu wa Pakistan Bw. Imran Khan, rais Xi amesema, China ina imani, uwezo na uhakika wa kushinda mapambano dhidi ya ugonjwa huo, na kufanya juhudi za kutimiza malengo ya maendeleo ya uchumi mwaka huu.

    Bw. Imran Khan amesema, kutokana na hatua za kinga na udhibiti za China, maambukizi ya virusi vya korona havijaenea duniani, na jamii ya kimataifa inapaswa kuishukuru China kutokana na juhudi na ufanisi wake katika kukabiliana na ugonjwa huo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako