• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • KASHFA: Rais wa PSG ashitakiwa kwa ufisadi

    (GMT+08:00) 2020-02-21 08:24:13

    Bosi wa Paris Saint-Germain Nasser Al-Khelaifi pamoja na katibu mkuu wa zamani wa Fifa Jerome Valcke wameshtakiwa rasmi Uswisi kwa madai ya ufisadi ya haki ya kutangaza michuano ya soka. Mwandesha mashtaka mkuu wa ofisi ya Uswisi(OAG) kwenye taarifa yake aliyoitoa Alhamis amesema wawili hao wanashtakiwa kwa kujihusisha na kutoa na kupokea haki za vyombo vya habari kutangaza makombe mbalimbali ya mashindano ya dunia na Mashirikisho ya Fifa. Mtuhumiwa wa tatu ambaye hakutajwa jina lake, ambaye ameelezewa na waendesha mashtaka wa Uswisi kama ni mfanyabiashara katika sekta ya haki za michezo, pia naye ameshtakiwa. Al-Khelaifi, ambaye pia ni bosi wa chaneli ya michezo ya televiseheni BeIN Sports ya Qatari anashutumiwa kwa kumpatia takrima Valcke yakiwemo makazi ya kifahari bila kulipa kodi ili atoe haki ya kutangaza michuano mikubwa ikiwemo kombe la dunia. Valcke, ambaye alikuwa msaidizi wa rais wa Fifa wa zamani Sepp Blatter, anashutumiwa kutoa haki na badala yake kupewa hongo. Kwa upande wake Bosi wa PSG amesema anatarajia kuafisha jina juu ya mashtaka hayo. Al-Khelaifi, amesema waendesha mashtaka wa Uswisi tayari wameshafuta mashtaka yanayohusiana na makombe ya Dunia ya 2026 na 2030.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako