• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kampuni za Marekani kuwekeza dola bilioni 2 Angola

    (GMT+08:00) 2020-02-21 18:56:58

    Makampuni kadhaa ya Marekani yatawekeza zaidi ya dola bilioni 2 katika miradi ya mafuta na gesi asilia, nchini Angola.

    Kwenye ziara nchini humo waziri wa mambo ya kigeni wa Marekani Mike Pompeo amekutana na Chama cha Biashara cha Angola, na kusema kuwa Marekani inapania kuwa mshirika muhimu kwa watu wa Angola.

    Pompeo amesema Marekani pia itaunga mkono juhudi za rais Rais João Lourenço za kuwa na uwazi wa uchumi na mapambano dhidi ya rushwa .

    Rais Lourenço alisema kuwa uwekezaji wa kibinafsi, usalama wa kikanda, vita dhidi ya ufisadi na kurejesha utajiri wan chi ulioibwa vipaumbele vya serikali yake.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako