• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kenya: Tuskys kupunguza wafanyakazi

    (GMT+08:00) 2020-02-21 18:57:18

    Maduka makubwa ya Tuskys nchini Kenya yametangaza kuwa yatapunguza wafanya kazi wake baada ya kuendelea kupungua kwa mauzo na wateja.

    Tuskys aliarifu wafanyikazi walioathirika wiki hii ikisema itapanga upya idara zake kujikinga kutokana na athari za hasara.

    Katika barua kwa Chama cha wafanyikazi kwenye sekta ya Tuskey imesema kuwa imelazimika kutangaza hatua ya kupunguza nguvu kazi ili kuendelea kuwa kwenye biashara.

    Haijabainika ni wafanyikazi wangapi wataathiriwa na upunguzaji huo utaanza kutekelezwa mwezi Machi.

    Tuskys pia imekuwa ikikabiliwa na ushindani unaokua kutoka kwa wauzaji wa ndani kama vile Naivas na Quickmart na wawekezaji wa kimataifa kama Game, Shoprite na Carrefour.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako