• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Tanzania: NMB kutoa huduma za bima

    (GMT+08:00) 2020-02-21 18:59:36

    Benki ya NMB nchini Tanzania imeanza kutoa huduma za bima katika matawi yake yote 224.

    Huduma hii imefuatia uzinduzi wa huduma ya bima kupitia benki (Bancassurance) uliofanyika juzi jiji Dar es Salaam.

    Huduma za bima zitakazopatikana katika matawi ya Benki ya NMB ni zile za kampuni za Sanlam Life, UAP, Shirika la Bima la Taifa (NIC), Jubilee, Shirika la Bima la Zanzibar (Zanzibar ( ZIC) na Reliance.

    Akizungumza katika uzinduzi huo, Meneja Mwandamizi wa Bima wa Benki ya NMB, Martin Massawe, alisema uwapo wa matawi ya benki yake katika wilaya zote nchini kutasaidia kukuza sekta ndogo ya bima na kuinua mchango wake katika pato la taifa.

    Hivi sasa sekta ndogo ya bima zinazosimamiwa na Mamlaka ya Bima nchini, huchangia asilimia 0.7 ya pato la taifa.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako