• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Rais Xi Jinping asisitiza udhibiti wa COVID-19 na maendeleo ya kiuchumi na kijamii

    (GMT+08:00) 2020-02-23 21:08:00

    Rais Xi Jinping wa China jana alihudhuria mkutano wa kuboresha kazi ya kuratibu kuzuia na kudhibiti ugonjwa wa virusi vipya vya korona (COVID-19) na maendeleo ya kiuchumi na kijamii uliofanyika mjini Beijing kwa njia ya simu.

    Mkutano huo umeendeshwa na waziri mkuu wa China Li Keqiang na kuhudhuriwa na Li Zhanshu, Wang Yang, Wang Huning, Zhao Leji na Han Zheng.

    Rais Xi amesema tangu mlipuko wa COVID-19 utokee, kamati kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China imechukua hatua madhubuti ili kudhibiti maambukizi ya virusi, na hadi sasa hatua hizo zimepata ufanisi. Amesema athari ya COVID-19 kwa uchumi wa China ni ya muda mfupi, na kudhibitika.

    Habari nyingine zinasema China itaongeza mshahara na marupurupu kwa madaktari na wauguzi haswa wale wanaotoa huduma mjini Wuhan na katika sehemu nyingine mkoani Hubei.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako