• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kenya yahimiza haja ya kuwawezesha wanawake

    (GMT+08:00) 2020-02-24 20:10:51

    Benki ya dunia imeitaka Kenya kutoa shinikizoa Zaidi katika kuwawezesha wanawake kiuchumi ili wachangie katika maendeleo ya nchi.

    Hayo yalisemwa wakati wafanyakazi 28 wa kike wahitimu walipopokezwa vyeti vya uongozi katika sekta ya huduma ya maji katika sherehe iliyofanyika katika hoteli ya Radisson Blu jijini Nairobi.

    Mradi huo uliofadhiliwa na Benki ya Dunia ulihusisha washiriki kutoka maeneo ya Pwani na Kaskazini Mashariki ambapo washiriki walihitimu baada ya kusomea kozi ya miezi sita katika masuala ya uongozi wa huduma katika sekta mbali mbali za maji na usafi.

    Akizungumza katika hafla hiyo, msimamizi wa utendaji wa Benki ya Dunia nchini Kenya Camille Lampart, alisema kwamba mashirika mema ni yale yanayotoa mazingira yanayowawezesha wafanyakazi wake kuonyesha uwezo wao kikazi.

    Kwa upande wake, Dkt Patricia Murugami, mwanzilishi na afisa mkuu mtendaji wa Breakthrough Leadership Transformation Group ambalo pia lilihusika katika maandilizi ya kozi hii, alisema kwamba mradi huo umewaruhusu washiriki kutambua uwezo wao wa uongozi.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako