• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • SOKA: Timu ya kinadada wa China "Steel Roses" yafufua matumaini ya wachina baada ya kutoshindwa kwenye mechi zake

    (GMT+08:00) 2020-02-25 09:25:13

    Timu ya mpira wa miguu ya wanawake nchini China imeibuka na kuonesha ishara ya kushinda virusi vya korona baada ya kutoka kwenye karantini na kukaribia kujikatia tiketi ya kucheza Olimpiki ya Tokyo. Wakati michezo ikiwa imesimamishwa kwa sababu ya mlipuko wa virusi, ambao umesababisha zaidi ya watu 2,500 kufariki nchini, timu hiyo imefufua matumaini na ufahari wa taifa. Licha ya kuwekwa karantini baada ya kufika Australia kwa mashindano ya kufuzu ambapo walifanya mazoezi kwenye koridoo za hoteli yao na kukimbia ngazini ili kujiweka fiti kina dada hao almaarufu kama Marose ya Chuma "Steel Roses" walicheza bila kushindwa huku wakitoka sare ya 1-1 dhidi ya Australia na kuifanya China icheze mechi ya mtoano dhidi ya Korea Kusini. Rikodi ya "Steel Roses" ya kutoshindwa mechi zake kwenye michuano ya kufuzu Olimpiki, imeng'arisha mioyo ya wachina kufuatia mlipuko.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako