• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mfumuko wa bei wapungua EAC

    (GMT+08:00) 2020-02-25 18:04:45

    Mfumuko wa bei kwa nchi za Afrika Mashariki (EAC)umepungua.

    Nchini Kenya, umepungua kwa asilimia 0.04, Uganda kwa asilimia 0.2 na Tanzania kwa asilimia 0.1, kwa mwezi Januari mwaka huu, ikilinganishwa na Desemba mwaka uliopita.

    Akizungumza jijini Dodoma siku chache zilizopita, kaimu Mkurugenzi wa Sensa ya Watu na Makazi wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS), Ruth Minja, alisema kupungua kwa mfumuko huo kunaonesha kwamba kasi ya mabadiliko ya bei za bidhaa na huduma kwa Januari mwaka huu, imepungua ikilinganishwa na mwezi Desemba mwaka jana.

    Alisema mfumuko wa bei wa taifa kwa Tanzania, umepungua kwa asilimia 0.1 kutoka asilimia 3.8 Desemba mwaka jana, hadi asilimia 3.7 Januari mwaka huu.

    Mfumuko wa bei nchini Kenya umepungua kwa asilimia 0.04 kutoka asilimia 5.82 Desemba mwaka jana, hadi asilimia 5.78 Januari mwaka huu.

    Kwa upande wa Uganda, alisema kwamba mfumuko wa bei umepungua kwa asilimia 0.2, kutoka asilimia 3.6 Desemba mwaka jana, hadi asilimia 3.4 Januari mwaka huu.

    Minja alisema kupungua kwa mfumuko wa bei mwezi Januari, kumechangiwa na kupungua kwa bei za baadhi ya bidhaa za vyakula na bidhaa aisizo za vyakula kwa Januari mwaka huu, ikilinganishwa na mwezi waDesemba mwaka jana.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako