• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Rais aahidi kutekeleza mapendekezo ya sukari

    (GMT+08:00) 2020-02-25 18:05:30

    Rais Uhuru Kenyatta ameahidi kuwa serikali yake itatekeleza mapendekezo ya jopokazi kuhusu sukari kama sehemu ya juhudi zinazoendelea za kufufua sekta hiyo.

    Rais alitoa hakikisho hilo mapema wiki hii katika Ikulu ya Nairobi, alipopokea ripoti ya jopokazi hilo ambalo aliliteua kuangazia sekta hiyo ya sukari.

    Rais Kenyatta aliliambia jopokazi hilo linaloongozwa na Waziri wa Kilimo Peter Munya, pamoja na Gavana wa Kaunti ya Kakamega Wycliffe Oparanya, kwamba serikali iko makini kuhakikisha wakulima wa miwa nchini wananufaika kutokana na kilimo chao.

    Mapendekezo makuu ya ripoti hiyo ni kuanzishwa tena kwa ushuru wa sukari, kubinafsishwa kwa viwanda vya umma ili kuboresha utendakazi pamoja na kubuniwa kwa sheria kuhusu sukari.

    Ushuru huo wa sukari utatozwa watumiaji ili kuwe na pato linalohitajika kuwasaidia wakulima.

    Mapendekezo mengine ambayo yamewasilishwa ni pamoja na kuchapishwa kwa kanuni za sekta ya sukari katika gazeti rasmi la serikali ikiwemo kuhusu uagizaji sukari kutoka mataifa ya kigeni, na kubadilishwa kwa utaratibu wa kutoza ushuru katika sekta hiyo ili kuboresha marupurupu kwa wawekezaji.

    Jopokazi hilo pia limependekeza kwamba kanuni za shirika la COMESA zitekelezwe kikamilifu.

    Kuhusu ubinafsishaji, Rais Kenyatta aliyeandamana na Naibu Rais William Ruto, alisema serikali haihitaji kuhusika katika biashara ya sukari kwa sababu wajibu wake ni kuwasaidia wakulima kupata mbegu bora, mbolea ifaayo na pembejeo muhimu za kilimo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako