• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mpango maalumu wa kukusanya maziwa kuanzishwa

    (GMT+08:00) 2020-02-25 18:05:52

    Kituo cha Kuendeleza Kilimo Endelevu cha Sustainable Agriculture Tanzania (SAT), kilichopo mkoani Morogoro, kinatarajia kuanzisha mpango maalumu wa kukusanya maziwa kisha kuyachakata na kuyauza ili kuongeza idadi ya wanywaji wa maziwa na kipato kwa wafugaji nchini.

    Akizungumza na waandishi wa habari mwishoni mwa wiki Ofisa kutoka SAT, Kashingye Salum alisema unywaji maziwa unatishia usalama wa afya za wananchi wengi kwakuwa kiwango cha mtu mmoja kunywa maziwa kwa mwaka ni lita 400 lakini wengi wana wastani wa lita 47 kwa mwaka jambo ambalo ni hatari kiafya na jitihada za haraka zinatakiwa kuchukuliwa ili kuongeza lita za unywaji kwa mwaka.

    Salum alisema Serikali imeweka mikakati kadhaa kuhakikisha unywaji maziwa unafikia angalau kiwango cha lita 200 kwa mwaka na ndio maana imepandisha hata kodi za maziwa yanayotoka nje ya nchi ili kuchochewa soko la ndani.

    Alisema Tanzania ina mifugo mingi lakini uzalishaji wake ni mdogo na ndio maana SAT kwa kushirikiana na Chuo cha Kilimo Sokoine (SUA), mikakati na tafiti mbalimbali ili kuwaendeleza wakulima na wafugaji.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako