• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China kusaidia Afrika kupambana na COVID-19

    (GMT+08:00) 2020-02-25 19:49:18

    Msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya China Zhao Lijian amesema, China itaendelea kutekeleza makubaliano yaliyofikiwa katika mikutano ya "Ukanda Mmoja, Njia Moja" na Baraza la Ushirikiano kati ya China na Afrika, na kutoa misaada kadri iwezavyo kwa nchi za Afrika zenye mfumo duni wa kiafya katika kupambana na maambukizi ya virusi vipya vya korona COVID-19.

    Mkurugenzi mkuu wa Shirika la Afya Duniani (WHO) Tedros Ghebreyesus ameeleza wasiwasi wake kuwa, maambukizi ya korona yanaweza kutokea katika nchi zenye mfumo duni wa afya, na kuitaka jamii ya kimataifa kutoa misaada kwa nchi hizo.

    Zhao amesema, wakati China inapokabiliana na COVID-19, nchi za Afrika ziliiunga mkono mara moja China na kutoa misaada, na China itazisaidia nchi hizo kuimarisha usalama wa afya wa kikanda na kimataifa.

    Akizungumzia mlipuko wa COVID-19 nchini Japan na Korea ya Kusini, Zhao amesema China inafuatilia sana maendeleo ya maambukizi ya virusi katika nchi hizo, na inapenda kuongeza mawasiliano na uratibu, na kuchukua hatua zipasazo kuzuia kuenea kwa maambukizi ya virusi.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako