• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Rwanda: Coronavirus kuaathiri uchumi wa Rwanda

    (GMT+08:00) 2020-02-26 19:18:22

    Coronavirus imeonekana kuwa moja ya mshtuko mkubwa unaoathiri uchumi wa dunia na inaweza kuwa na athari kwa uchumi wa ndani, wachumi wameonya.

    Kwa Rwanda, wachumi wanasema, baadhi ya athari zinaweza kuonekana katika utaftaji wa bidhaa zinazotumika katika soko la ndani.

    Gavana wa Benki ya Kitaifa ya Rwanda John Rwangombwa amesema kwamba wastani wa asilimia 20 ya uagizaji wa Rwanda utoka China.

    Uchumi wa Rwanda utaathirika pakubwa pale kunatarajiwa kuwa uhaba wa bidhaa bidhaa katika soko la ndani.

    Hii inaweza pia kuathiri maendeleo katika miradi kadhaa ambapo bidhaa za mitaji na maendeleo ya viwanda ambapo malighafi hutolewa China.

    Wafanyibiashara wamesema wanatarajia mizingo ambayo ilikuwa imeagizwa hapo awali, lakini hawana uhakika wanaweza kupata bidhaa kutoka china siku za baadaye, hivyo itawalazimu kutafuta njia mbadala na hiyo ni kununua kuagiza biadha kutoka Dubai iwapo gharama yake ni kubwa mno ikilinganishwa na China.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako