• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Ubadilishaji fedha kiholela katika mpaka wa Tunduma na Tanzania ya tarajiwa kuisha baadaya ya Benki Kuu za nchi hizo kukubaliana Shilingi na kwacha kutumika kwenya biashara

    (GMT+08:00) 2020-02-26 19:19:26

    Ubadilishaji fedha kiholela katika mpaka wa Tunduma unaotenganisha Tanzania na nchi jirani ya Zambia unatarjiwa kuwa historia baada ya Benki Kuu za nchi hizo kukubaliana Shilingi na kwacha kutumika kwenya biashra za kuuziana bidhaa kwenye maeneo ya Tunduma na Nakonde.

    Hatua hiyo ni kuhakikisha hakuna vijana watakaoendlea kuzurura kwenye miji ya Tunduma na Nakonde wakiwa wameshika vibunda vya noti za fedha za shilingi za Tanzania, Kwacha ya Zambia na Dola ya Marekani.

    Mkurungezi mkuu wa Benki Kuu Ya Tanzania Tawi la Mbeya Ibrahim Malogoi amesema Benki Kuu za nchi zote mbili utratibu wa matumizi ya shilingi ya Kwacha utazinduliwa rasmi na kuanza kutumika kwenye miji hiyo iliyo na pilikapilika za kibiashara.

    Faida zitakazopatikana kupitia mfumo huo ni kuondoa kabisa gharama za ubadilishaji fedha kwa kuwa mwananchi mwenye Kwacha na anahitaji shilingi halazimiki tena kuibadilisha kupitia dolaya Marekani.

    Pia itachochea biashara kwa kuwa sasa wafanyibiashara wan chi hizo mbili hawatalazimika kubadilisha fedha zao.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako