• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China yasema inapinga shutuma zisizo za msingi zinazotolewa na waziri wa mambo ya nje wa Marekani

    (GMT+08:00) 2020-02-26 19:34:46

    Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya China Zhao Lijian amesema China inapinga kithabiti shutuma zisizo na msingi zinazotolewa na waziri wa mambo ya nje wa Marekani Mike Pompeo dhidi yake, na kumtaka aache kuharibu uhusiano kati ya Chama cha Kikomusniti cha China CPC, serikali, na watu wa China.

    Habari zinasema, Pompeo jana alisema hatua ya serikali ya China "kuwafukuza" waandishi wa habari wa gazeti la The Wall Street Journal imeonesha mapungufu ya China katika kushughulikia habari kuhusu maambukizi ya virusi vya korona COVID-19.

    Kuhusu kauli ya balozi Sam Brownback wa Marekani anayeshughulikia masuala ya dini kuwa, hatua ya China ya kuwafanya waislamu wa Xinjiang kuwa "raia bora wanaopenda amani" ni vita ya kidini, Zhao Lijian amesema serikali ya China inalinda uhuru wa kuabudu wa raia wake kwa mujibu wa sheria. Amesema kuna misitiki zaidi ya elfu 24 mkoani Xinjiang, idadi ambayo ni mara kumi zaidi kuliko idadi ya misikiti yote nchini Marekani. Amemtaka balozi huyo awajibike na kuacha kuingilia kati mambo ya ndani ya China kwa kutumia suala la dini.

    Wakati huohuo, Bw. Zhao amesema serikali ya China inatoa salamu za rambirambi kufuatia kifo cha aliyekuwa rais wa Misri Hosni Mubarak.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako