• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • TENISI: Maria Sharapova ataafu rasmi mchezo wa tenisi

    (GMT+08:00) 2020-02-27 08:54:36

    Bingwa mara tano wa Grand Slam Maria Sharapova ameuaga rasmi mchezo wa tenisi akiwa na umri wa miaka 32. Kwenye makala iliyoandikwa na Vogue and Vanity Fair, Sharapova amesema mwili wake umekuwa dhoofu baada ya kuteseka na majeraha ya bega. Mrussia huyo alishinda Grand Slam yake ya kwanza Wimbledon mwaka 2004 akiwa na umri wa miaka 17 na kumaliza kibarua chake cha Grand slam kwa kushinda Michuano ya wazi ya Ufaransa mwaka 2012. Mwaka 2016, alitumikia marufuku yake ya miezi 15 baada ya vipimo kuonesha anatumia meldonium. Baada ya kumaliza marufuku yake mwaka 2017, Sharapova alijitahidi kurejesha uwezo wake wa awali na kupata majeraha mengi. Aliporomoka na kuwa wa 373 katika kiwango cha dunia, kikiwa ni kiwango kidogo zaidi tangu Agosti 2002, na amekuwa akishindwa katika raundi ya kwanza kwenye miaka mitatu iliyopita ya mashindano yake ya Grand Slam.
    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako