• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China yapinga kithabiti lawama zisizo na msingi kwa masuala yanayohusu mkoa wa Xinjiang

    (GMT+08:00) 2020-02-27 09:55:43

    Mjumbe wa kudumu wa China katika ofisi za Umoja wa Mataifa na mashirika mengine ya kimataifa mjini Geneva, Uswizi Bw. Chen Xu amehutubia mkutano wa 43 wa Baraza la Haki za Binadamu la Umoja wa Mataifa, akisema baadhi ya nchi zinafuata msimamo wenye upendeleo na makosa dhidi ya China, zikiilaani China kwa masuala yanayohusu mkoa wa Xinjiang kwenye mkutano huo. Amesema China inapinga kithabiti na kamwe haikubali kitendo kama hicho.

    Bw. Chen Xu ameeleza kuwa, China imechukua hatua mbalimbali za kupambana na ugaidi na kuondoa itikadi kali za kidini ikiwemo kujenga kituo cha mafunzo ya ufundi stadi, hatua ambazo zimeboresha hali ya usalama wa mkoa huo, kulinda haki za kibinadamu za watu wanaoishi mkoani humo, na pia kutoa mchango mkubwa katika mapambano ya kimataifa dhidi ya ugaidi na kuondoa itikadi kali za kidini. Pia ameeleza kuwa China inapenda kuwaalika wageni wengi zaidi kutembelea mkoa wa Xinjiang ili waweze kushuhudia maendeleo ya uchumi, jamii na mambo ya haki za kibinadamu mkoani humo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako