• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kampuni ya umeme ya Kenya Power yaandikisha utendaji mbaya katika kipindi cha miaka 16

    (GMT+08:00) 2020-02-27 18:34:13
    Kampuni ya umeme ya Kenya Power imetangaza faida yake mbovu ndani ya miaka 16, na kulekeza malengo yake katika kushinikiza ongezeko la bei ya umeme kwa wateja wa rejareja na biashara.

    Faida halisi ya kampuni hiyo ilishuka kwa silimia 92 kutoka Sh3.26 bilioni hadi Sh262 milioni katika kipindi cha mwaka fedha kufikia Juni — faida ya chini kabisha tangu kurejea katika utengenezaji faida mwaka 2004 baada ya kuandikisha hasara ya Sh2.89 bilioni mwaka kabla ya huo.

    Kampuni ya Kenya Power imesema gharama za kununua umeme kutoka kwa wazalishaji kama vile KenGen ziliongezeka kwa Sh18 bilion katika kipindi hicho.

    Aidha kampuni ya Kenya Power imetuma ombi la kwa mdhibiti wa nishati kuongeza bei ya umeme , ikisema kuwa ni muhimu katika kuiingizia faida.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako