Akiwasilisha hotuba ya mwelekeo wa hali ya uchumi ,mpango wa maendeleo na bajeti kwa mwaka 2020/21 -2022/23 jana, katika ukumbi wa Baraza la Wawakilishi , Waziri wa Fedha na Mipango Balozi Mohammed Ramia alisema ongezeko hilo linatokana na matarajio ya kuongezeka kwa wawekezaji wa miradi ya maendeleo .
Balozi Ramia alisema mapato ya ndani kwa kipindi cha miaka mitatu yanakadiriwa kufikia asilimia 26.0 ya Pato la Taifa kwa miaka 2019 -2022 kutoka wastani wa asilimia 24.2 ya mwaka 2018/19.
Wakichangia hotuba hiyo,wajumbe wa Baraza la Wawakilishi waliishauri serikali kuweka kipaumbele katika miradi ya maendeleo itakayosaidia kuongeza uchumi na Pato la Taifa.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |