• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Serikali ya Tanzania imekamilisha mipango ya kujenga kiwanda kikubwa cha Vifaa Tiba

    (GMT+08:00) 2020-02-27 18:35:07
    Serikali ya Tanzania imekamilisha mipango ya kujenga kiwanda kikubwa cha vifaa tiba, kuchakata pamba na bidhaa zinazotokana na zao hilo mkoani Simiyu ili kuongezea thamani ya zao hilo na kukuza soko la ndani na nje nchi.

    Hayo yalibainishwa jana na Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu(Uwekezaji), Angela Kairuki, mjini humo , na kueleza kuwa sambamba na hilo kiwanda hicho ambacho jiwe lake la msingi litawekwa Mei mwaka huu, kitamaliza kabisa tatizo la uingizaji wa vifaa tiba kutoka nje.

    Akizungumza katika mkutano wa majadiliano kati ya sekta ya umma, wawekezaji na wafanyabiashara katika Mkoa wa Simiyu uliolenga kujadili changamoto na kupata mapendekezo yatakayosaidia kuboresha mazingira ya kufanya biashara na uwekezaji jana, Kairuki alisema serikali imeyapa kipaumbele mazao ya kimkakati ikiwamo zao la pamba.

    Alisema lengo la serikali ni kupunguza uagizaji wa bidhaa na pia usafirishaji wa malighafi nje ya nchi jambo linaloikosesha nchi mapato stahiki na

    kupunguza uwezo wa wawekezaji wa ndani kushindana na kukuza mitaji yao ya uwekezaji.

    Alisema azma ya serikali ya kufikia uchumi wa kati na viwanda itafanikiwa tu pale bidhaa kutoka nje zitapungua na ndiyo

    itakuwa silaha ya kuvilinda viwanda vya ndani.

    Aidha Kairuki alitoa wito kwa Soko la Hisa la Dar es Salaam (DSE) kuangalia namna bora ya kufikisha huduma pande zote za nchi ili kutoa fursa ya wananchi kuwekeza katika soko la hisa kwa lengo la kukuza mitaji.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako