• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Balozi wa China katika Umoja wa Mataifa apinga tuhuma zisizo na msingi kuhusu masuala ya Xinjiang

    (GMT+08:00) 2020-02-27 19:52:12

    Balozi wa kudumu wa China katika Ofisi za Umoja wa Mataifa mjini Geneva Bw. Chen Xu amepinga tuhuma zinazotolewa na baadhi ya nchi za Magharibi dhidi ya China kuhusu masuala ya mkoa wa Xinjiang.

    Balozi Chen amesema hayo kwenye mkutano w 43 wa Baraza la Haki za Binadamu la Umoja wa Mataifa, na kusema serikali ya China imepokea wanadiplomasia, maafisa wa mashirika ya kimataifa, waandishi wa habari na viongozi wa kidini waliotembelea mkoani Xinjiang, ambao wamesema kile walichokiona katika mkoa wa Xinjiang ni kinyume kabisa na taarifa zinazotolewa na baadhi ya vyombo vya habari vya nchi za Magharibi.

    Balozi Chen amesema China imechukua hatua kadhaa kupambana na ugaidi na msimamo mkali, ikiwemo kuanzisha vituo vya elimu vya ufundi na mafunzo mkoani Xinjiang, ambavyo vimeboresha usalama mkoani humo, kulinda haki za makabila yote na kutoa mchango kimataifa katika kupinga ugaidi na msimamo mkali.

    Wakati huohuo, mwakilishi maalumu wa wizara ya mambo ya nje anayeshughulikia haki za binadamu Bw. Liu Hua amesema, ulinzi wa haki za binadamu hauna kiwango cha dunia, na ni lazima uzingatiwe kikamilifu kuendana na hali ya kitaifa kwa kufuata kanuni ya sheria ya Umoja wa Mataifa na roho ya mkataba wa haki za binadamu.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako