• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mtaalamu wa China asema, COVID-19 kudhibitiwa kabisa nchini China April

    (GMT+08:00) 2020-02-27 20:02:17

    Kiongozi wa tume ya watalaamu ya kukabiliana na mlipuko wa ugonjwa huo Dokta Zhong Nanshan amesema, China ina imani kuwa, mlipuko wa virusi vya korona (COVID-19) utadhibitiwa kabisa itakapofika mwisho wa mwezi Aprili.

    Akizungumza na wanahabari mjini Guangzhou, Dokta Zhong amesema, awali ugonjwa huo ulipoanza kuenea, wataalamu wa nchi za nje walitabiri kuwa, wagonjwa wangefikia laki 1.6 mwanzoni mwa Februari, na hali haitadhibitiwa kabla ya mwisho wa mwezi May. Daktari Zhong amesisitiza kuwa, utabiri huo ulitolewa bila kufahamu kuwa, serikali ya China ingeweza kuchukua hatua kali za kuzuia kuenea kwa virusi, ambazo tayari zimeanza kupata mafanikio.

    Vile vile Daktari Zhong amesema, huenda China si chanzo cha virusi hivyo, ingawa kesi ya kwanza ya ugonjwa iliripotiwa nchini China, kwani nchi nyingine pia zimeanza kutoa ripoti kuhusu kuwepo kwa wagonjwa ambao haijafahamika waliambukizwa kwa njia gani.

    Mtaalamu huyo ambaye atakuwa na warsha kupitia vido na wataalamu husika wa Ulaya na kutoa uzoefu wa China katika kupambana na virusi hivyo, amesema ugonjwa huo ni tatizo la binadamu, sio la nchi moja tu, hivyo ushirikiano wa kimataifa unahitajika.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako