• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Rais wa China asema China na Mongolia zinasaidiana kukabiliana na changamoto

    (GMT+08:00) 2020-02-27 20:11:05

    Rais Xi Jinping wa China amefanya mazungumzo na mwenzake wa Mongolia Khalmaa Battulga leo hapa Beijing.

    Rais Xi amesema serikali ya China na watu wake wanafanya juhudi zote kupambana na mlipuko wa virusi vipya vya korona, ambapo serikali ya Mongolia na wananchi wake wametoa uungaji mkono muhimu.

    Amesema Battulgani ni rais wa kwanza kufanya ziara nchini China tangu mlipuko huo kutokea. Ikiwa na lengo la kutoa salamu na uungaji mkono kwa China, ziara hiyo imeonesha mkazo mkubwa unaotiliwa na rais huyo kwa uhusiano kati ya nchi yake na China, na urafiki mkubwa kati ya watu wa nchi hizo mbili. Rais Xi ameongeza kuwa ziara hiyo ni ushahidi kuwa nchi hizo jirani ziko katika meli moja na zinajitahidi kusaidiana.

    Kwa upande wake, rais Battulgani amesema akufaaye kwa dhiki ndiye rafiki, watu wa Mongolia wako pamoja na majirani zao wa China katika kukabiliana na changamoto za sasa.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako