• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kiongozi wa tume ya kupambana na virusi vya Korona China asisitiza umuhimu wa ushirikiano wa kimataifa

    (GMT+08:00) 2020-02-28 09:04:44

    Kiongozi wa tume ya watalaamu ya kukabiliana na mlipuko wa virusi vya COVID-19, Dokta Zhong Nanshan, amesema ni lazima kuimarisha ushirikiano wa kimataifa kuhusu kinga na udhibiti wa maambukizi ya virusi vya korana.

    Akizungumza na wanahabari mjini Guangzhou, Dokta Zhong amesema hivi sasa ongezeko la maambukizi mapya katika nchi za nje limezidi ongezeko la maambukizi mapya nchini China, hasa katika nchi za Korea Kusini, Iran na Italia, ambapo virusi hiyo vinaenea kwa kasi, labda hatua za China zinaweza kuigwa na nchi hizo. Kutokana na mwaliko, Dokta Zhong atatoa ripoti ya video kwa Taasisi ya Mfumo wa Kupumua ya Ulaya wikiendi hii.

    Vilevile Dokta Zhong amesisitiza kuwa maambukizi ya virusi vya korona ni ugonjwa wa binadamu, wala si ugonjwa wa taifa fulani. Amesema China ina imani kuwa, mlipuko wa virusi vya korona utadhibitiwa kabisa ifikapo mwisho wa mwezi Aprili.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako