• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • SOKA: Olympiakos yaiondoa Arsenal kwenye Ligi ya Europa

    (GMT+08:00) 2020-02-28 09:18:17

    Nahodha Pierre-Emerick Aubameyang amekosa nafasi ya wazi huku Arsenal wakishindwa kwenye Ligi ya Europa hatua ya 32 wakiwa mikononi mwa Olympiakos kwenye mtanange uliochezwa usiku wa kuamkia leo. Aubameyang, ambaye mara nyingi ndio anaonekana muokozi wa Gunners, kwa mara nyingine tena ilionekana ameiokoa timu yake baada ya kupachika mpira wavuni katika dakika ya 113 na kuweka mzani sawa wa goli 1-1 na kuwafanya washike usukani zikiwa zimesalia dakika saba za muda wa nyongeza. Lakini wageni wao waliamua kuwaadhibu wenyeji wao kwa kuongeza goli la pili dakika ya 119 lililoingizwa kimiani na Youssef El Arabi na kuleta shangwe kama lote mbele ya mashabiki wao wenye mbwembwe waliotoka nyumbani kwenda kuwashangilia. Arsenal sasa watakuwa wametolewa kwenye michuano baada ya kufungwa kwa goli la ugenini.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako