• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mradi wa ufugaji wa samaki wacheleweshwa na mzozo wa fidia

    (GMT+08:00) 2020-02-28 19:00:26
    Kucheleweshwa kwa fidia ya wamiliki wa ardhi kumesababisha kuchelewa kwa utekelezaji wa mradi wa ufugaji samaki katika Wilaya ya Apac nchini Uganda.

    Mradi huo unaofadhiliwa na Jumuiya ya Ulaya unatarajiwa kuajiri zaidi ya vijana 500 na pia mabwawa ya kufuga samaki kwa wenyeji ili kuwawezesha kuboresha mapato yao.

    Hata hivyo baadhi ya wakaazi katika vijiji vya Onekgwok na Teboke, wanasema kazi hazitaanza hadi wafidiwe kikamilifu ardhi yao.

    Jumla ya watu 18 walioathiriwa na mradi huo walidai ardhi yenye utata ya ekari ya 197, haikuchunguzwa lakini imejumuishwa chini ya ardhi ya jamii.

    Mwenyekiti wa wakaazi walioathiriwa Bwana Peter James Ocen anasema waliripoti kwa ofisi husika ili ardhi yaoichunguzwe, kuthaminiwe na tunalipwa lakini bado swala hilo halijatatuliwa.

    Naibu mwenyekiti wa Wilaya ya Apac, pia diwani wa kaunti ndogo ya Ibuje, Bwana Asanti Odongo, alisema wanachunguza suala hilo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako