• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Wafanyakazi Rwanda kuchangia zaidi kwa bima ya afya

    (GMT+08:00) 2020-02-28 19:00:43
    Wizara ya utumishi wa umma nchini Rwanda imesema wafanyikazi wote watapunguzwa sehemu ya mshahara wao ili kuongeza fedha za mpango wa bima ya afya ya msingi unaofahamika kama mutuelles de santé.

    Kulingana na taarifa kutoka kwa Wizara ya Utumishi wa Umma na Kazi, asilimia 0.5 ya mshahara wote utatolewa na mwajiri kila mwezi.

    Upunguzaji huo utaathiri wafanyikazi wa umma na wa kibinafsi.

    Hatua hiyo inaambatana na uamuzi wa Serikali wa kutekeleza ruzuku zaidi kwa mpango wa bima ya afya ambao umekuwa ukikabiliwa na uhaba wa fedha.

    Aliyekuwa Mkurugenzi Mkuu wa halmashauri ya haziza ya jamii Richard Tusabe, amesema fedha hizo za ziada zitasaidia kufanikisha mpango wa taifa wa bima ya afya kwa wote

    Kufikia sasa, mpango wa Bima ya Afya ya Jamii ni mpango mkubwa zaidi wa bima, unaohudumia asilimia 88 ya watu milioni 12 wa Rwanda kwa mahitaji yao ya huduma ya afya.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako