• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Wachimbaji kupata maboresho ya huduma za fedha

    (GMT+08:00) 2020-02-28 19:01:20

    Wachimbaji wadogo wa madini wameahidiwa kuboreshewa huduma za kifedha.

    Ahadi hiyo imetolewa na Benki ya NBC ambayo imejizatiti katika kuboresha huduma na bidhaa zake ziendane na mahitaji mahsusi ya wachimbaji wadogo.

    Ahadi hiyo imetokana na uzoefu ambayo benki hiyo imeupata wakati wa kongamano la madini, ambalo lilifadhiliwa na benki hiyo.

    Wakala wa Mauzo Kitengo cha Hazina na Masoko ya Fedha za Kigeni wa benki hiyo, Emmanuel Charles Gasirabo alisema kufuatia ufahamu wa ziada uliopatikana juu ya sekta hiyo, benki yake imeng'amua namna ya kujipanga kisawasawa ili kuhakikisha kuwa wanachangia kwa vitendo katika ukuaji wa sekta ya uchimbaji.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako